Tanzania ya pili utoaji chanjo ya Uviko-19 Afrika

HomeKitaifa

Tanzania ya pili utoaji chanjo ya Uviko-19 Afrika

Mratibu Kiongozi Kimataifa wa Ubia wa Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 Bw. Ted Chaiban ameipongeza Tanzania na nchini nyingine Barani Afrika pamoja na wadau wa Sekta ya afya kwa uhamasishaji na kuchanja wananchi chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Bw. Ted Chaiban amebainisha kuwa Tanzaina imeshika nafasi ya 2 kwa kiwango cha juu cha uchanjaji huku ikiwa imefikia asilimia 37.9 ya uchanjaji wananchi kwa mujibu wa takwimu za kidunia.

Katika kusisitiza hilo, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wadau wa maendeleo, Watumishi wa afya na watu wengine waliowezesha kufanikisha jitihada hizi za kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya 2 Afrika kwa kiwango cha juu cha uchanjaji.

error: Content is protected !!