Mgawanyo wa fedha za IMF kaa la moto kwa wakuu wa mikoa

HomeKitaifa

Mgawanyo wa fedha za IMF kaa la moto kwa wakuu wa mikoa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameanisha mgawo wa fedha Sh bilioni 535.6 kati ya Sh trilioni 1.3 ambazo serikali imepokea kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya kupambana na athari ya ugonjwa wa UVIKO-19

Katika hilo, amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha madarasa 12,000 ya sekondari na 3,000 ya vituo shikizi yanakamilika kabla ya Desemba 15, mwaka huu, ili wanafunzi wote watakaoanza masomo Januari wasikose madarasa wala viti vya kukalia.

“Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 304 ni kwa ajili ya elimu msingi, shilingi bilioni 226.68 ni kwa ajili ya afya ya msingi na shilingi bilioni 5.00 ni kwa ajili ya kuboresha miundombinu na mazingira ya kufanyia biashara kwa wafanyabiashara wadogo,” amesema.

Waziri Ummy amesema hayo jana jijini Dodoma wakati akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi na kuwaelekeza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha miradi ya ujenzi wa madarasa inakamilika kabla au ifikapo Desemba 15, mwaka huu na miradi mingine ikamilike ifakapo Aprili 30, mwakani.

error: Content is protected !!