Mita 111 za maji zajazwa Bwawa la Nyerere

HomeKitaifa

Mita 111 za maji zajazwa Bwawa la Nyerere

Serikali imesema hadi jana asubuhi, mita za maji 111 juu ya usawa wa bahari zilikuwa zimejazwa katika mradi wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme kwa maji katika bwawa la Nyerere kwenye bonde la Mto Rufiji.

Msemaji Mkuu wa Serikali. Gerson Msigwa alisema jijini Dodoma jana kuwa kazi ya ujenzi ipo zaidi ya asilimia 80 katika mradi huo unaotarajiwa kugharimu Sh trilioni 6.5.

“Tunaendelea kujaza hili bwawa ambalo litakuwa na uwezo wa kujaza maji lita bilioni 32, tunatarajia kulijaze kwa misimu miwili,”alisema.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, kwa mujibu wa wataalamu waji yakijaa kufikia mia 163 juu ya usawa wa bahari kazi ya kuzalisha umeme inaweza ikaanza.

 

 

 

error: Content is protected !!