Sh. milioni 150 zatengwa kujenga barabara korofi Iringa

HomeKitaifa

Sh. milioni 150 zatengwa kujenga barabara korofi Iringa

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Zainabu Katimba amesema serikali imeshaanza kujenga barabara korofi ya Ilula Image na Ibumu mkoani Iringa .

Akijibu swali bungeni mjini Dodoma , Katimba amesema tayari serikali imeshatoa fedha za dharura Sh Milioni 150, ili kujenga barabara hizo kurahisisha usafirishaji katika eneo hilo.

Katimba amesema serikali inatambua umuhimu wa barabara hizi katika suala zima la uzalishaji mali na ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.

Hatahivyo amesema barabara nyingine Kitoo, Masisiwe na Mwatasi nazo zilitengewa fedha shilingi Milioni 36.8 kwa lengo la kuchonga barabara kilomita 8 na kuweka kifusi kilomita 2.

error: Content is protected !!