Rais Samia azidi kuwawezesha wanawake na vijana

HomeKimataifa

Rais Samia azidi kuwawezesha wanawake na vijana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kutoa msaada wa kutosha kwa wajasiriamali wanawake na vijana ili kushiriki kikamilifu katika biashara na kutumia ipasavyo fursa zitonanazo na soko la Afrika.

Ametoa wito huo leo katika Kongamano la wanawake na vijana wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) lililofanyika kwenye ukumbi wa JNICC.

“Ninaomba viongozi wenzangu tuendelee kuwekeza zaidi katika rasilimali watu hususani wanawake na vijana, tukiwa na nguvu kazi imara yenye ujuzi wa kutosha tutatumia maliasili zetu vizuri hatimaye kuwezesha Afrika kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa dunia” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisema kwamba serikali ya Tanzania itaendelea kuwawezesha wanawake na vijana kutimiza malengo yao ya kibiashara.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwawezesha wanawake na vijana katika kutimiza malengo yao ya kibiashara chini ya mkataba huu tunaojadili hapa wa eneo huru la biashara la Afrika,” amesema Rais Samia Suluhu.

error: Content is protected !!