Mayele ampa mtoto bao

HomeMichezo

Mayele ampa mtoto bao

Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Fiston Mayele amesema bao alilofunga kwenye mechi ya Ligi Kuu juzi kati ya timu yake na Geita Gold amempa zawadi mtoto wake wa kwanza ambaye anasherekea siku yake ya kuzaliwa leo Machi 8. 

“Nashukuru sana kufunga bao hili, nampa mtoto wangu wa kwanza hili ni kwa ajili yake, nilimpigia simu nikamwambia nitafunga goli la zawadi kwa ajili yake na kweli nimefunga , nimefurahi sana,” alisema Mayele.

Mpaka sasa Mayele ndiye mchezaji anayeongoza kwa magoli mengi kwa kufikisha mabao 10 na huku akidai kwamba upinzani ni mkali na wote anaochuana nao wapo vizuri.

“Upinzani ni mkubwa sana ninaokimbzana nao ni mastraika wazuri. Mpole anacheza vizuri, Lusajo naye ni straika mzuri na nafasi ya ufungaji bado ni ngumu siwezi kusema lolote kwa sasa ika nashukuru nimefunga bao la 10,” alisema straika huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

error: Content is protected !!