Kizz Daniel atolewa Polisi na Harmonize

HomeBurudani

Kizz Daniel atolewa Polisi na Harmonize

Hatimaye mwimbaji wa muziki kutoka Nigeria, Kizz Daniel ametolewa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam alipokuwa amewekwa rumande. Msanii @harmonize_tz amemtoa mikononi mwa Polisi usiku na kuondoka nae.

Tukio hilo ambalo limeshuhudiwa na Bongo5, wameripoti kuwa, @harmonize_tz alifika kituoni hapo tangu majira ya saa 2 usiku na kutumia muda wa takribani saa moja na nusu kufanya mazungumzo na askari kituoni hapo na baadaye kuondoka na msanii huyo.

Itakumbukwa, mapema jana majira ya saa 10 alasiri, Kizz Daniel alikamatwa na kuwekwa rumande katika kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam, hii ni baada ya kushindwa kutokea kwenye show ya Summer Amplified aliyotakiwa kutumbuiza usiku wa kuamkia jana.

error: Content is protected !!