Uber na Bolt kurejesha huduma

HomeKitaifa

Uber na Bolt kurejesha huduma

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema, kampuni za usafiri kwa njia ya mtandao Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafiri nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, Septemba 12, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.

Latra wametoa taarifa hizo kipindi ambacho kampuni hizo kwa nyakati tofauti, walisitisha kutoa huduma za usafiri za magari na kubaki na bodaboda pamoja na bajaji.

Suluo amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari wamekubaliana kutatua tatizo ili kurejesha huduma.

“Tuliwaita wakaja na wawakilishi wao wa Afrika, tukaanza Septemba 5-8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tunataka watuletee kimaandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio mwisho wa mda tuliokubaliana na tutatoa maamuzi yatakayowasaidia wote wakiwemo umoja wa madereva teksi (TODA),” amesema mkurugenzi huyo.

 

error: Content is protected !!