Ajinyonga siku ya kwenda kutoa mahari

HomeKitaifa

Ajinyonga siku ya kwenda kutoa mahari

Dk Joseph Ngonyani anadaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka akiwa nyumbani kwake kitongoji cha Saghana na kuacha simanzi na vilio kwa ndugu na majirani.

Ngonyani aliyekuwa mfanyakazi wa zahanati ya Saghana iliyopo nje kidogo ya mji wa Himo Kata ya Makuyuni  wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, anadaiwa kujinyonga Jumamosi Novemba 26,2022, siku ambayo ilikuwa ni ya kupeleka mahari ukweni na ikiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya siku ya harusi yake Desemba 28.

Inaelezwa kuwa muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea ukweni kutoa mahari, aliwaambia aliokuwa aambatane nao, watangulie na yeye angewafuata, lakini kadiri muda ulivyokuwa ukienda na wao kukaribia ukweni, wakaanza kumpigia simu, ambayo iliita kwa juda bila majibu na baadaye ikawa haipatikani kabisa.

Mshenga wa Dk Ngonyani, Alex Athuman Mzee alisema baada ya kufika nyumbani kwa msichana, walitakiwa kutoa ng’ombe 10 na mbuzi 20 ambayo ni sawa na sh 4.6 milioni na kijana aliniambia yuko sawa na hakuna shida.

“Saa nne asubuhi ya siku ya Novemba 26 nikamtafuta kumwambia kuna kitu kitahitajika kitangulie, akanunua kikatangulia, saa saba nikamtafuta nikamwambia muda umeenda akaniambia kwa kuwa kuna kitu anasubiri, mimi na mama tuliokuwa tukienda tutangulie, atatufata, lakini yule mama akasema tusubirie., Saa nane nikampigia simu akasema anakuja twende na saa tisa ilipofika akawa hapatikani hadi kesho yake asubuhi naambiwa amefariki kwa kujinyonga,” alisema Athuman.

error: Content is protected !!