Rais Samia na Waziri Majaliwa wanunua tiketi 4000 mechi ya Taifa Stars

HomeKitaifa

Rais Samia na Waziri Majaliwa wanunua tiketi 4000 mechi ya Taifa Stars

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wametoa tiketi 4,000, kwa ajili ya mashabiki kuingia Uwanjani kwenye mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda, utakaopigwa Machi 28, mwaka huu.

Akizungumza kwa njia ya simu, Waziri Mkuu amesema Rais Samia anachangia tiketi 2000 na yeye atachangia 2000.

“Mheshimiwa Rais amenipigia simu amesema yeye pamoja nasi anachangia tiketi 2000,” amesema Waziri Mkuu.

Hivi karibuni, Rais Samia amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo nchi hasa mpira wa miguu baada ya kutoa ahadi ya kununua magoli kwa timu za Simba SC na Yanga ili kuwapa ari ya kufanya vizuri zaidi.

 

error: Content is protected !!