Waziri Mkuu amsimamisha kazi mtumishi aliyekutwa na sare za jeshi

HomeKitaifa

Waziri Mkuu amsimamisha kazi mtumishi aliyekutwa na sare za jeshi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amemsimamisha kazi Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Kibiti, Goefrey Haule, kwa tuhuma za rushwa na kukutwa amevaa sare za jeshi akitapeli wananchi.

Majaliwa alimsimamisha kazi Haule jana wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo mkoani Pwani.

Alisema ofisa huyo alikutwa wilayani Kilwa akiwa amevaa sare za jeshi akijifanya ofisa anayeshughulikia ajira za vijana katika mradi wa gesi wa Songosongo.

Majaliwa alisema ofisa huyo alichukua rushwa kwa vijana waliokuwa wanakwenda katika mradi huo wa Songosongo, lakini wakawa hawatambuliki ndiyo maana alikamatwa.

“Nilipomhoji alikataa na alipohojiwa na maofisa wetu alikubali kufanya vitendo hivyo,” alisema.

Waziri Mkuu alisema juzi ofisa huyo alikamata wavuvi watano wakifanya uvuvi haramu na kuwaandikia mashataka yaliyowatakata kulipa faini Sh. milioni 10 lakini walichukua rushwa ya sh. milioni tatu na kugawana na wenzake ambao ni polisi na mtendaji wa kijiji.

Hivyo, Majaliwa alimwagiza ofisa utumishi wa halmashauri hiyi kumwandikia barua ya kumsimamisha kazi Haule.

Mbali na hatu hiyo, Waziri Mkuu aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ofisa huyo.

 

 

error: Content is protected !!