“Mdogo wangu Mwinyi, simama kama mbuyu.”- Rais Samia

HomeKitaifa

“Mdogo wangu Mwinyi, simama kama mbuyu.”- Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka familia ya hayati Ali Hassan Mwinyi kuendelea kuheshimiana na kushikamana na kwamba hawatafurahi kuona familia hiyo inakinzana, ina migogoro na haiheshimiani.

Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 02, 2024 akitoa salamu za pole kwa familia ya hayati Mzee Mwinyi, Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania aliyefariki dunia Februari 29, 2024 kutokana na maradhi ya saratani ya mapafu.

Akizungumza Rais Samia amesema, “Mdogo wangu Hussein, simama kama mbuyu, na mbuyu huu uende ukaheshimike,” amesema Rais Samia na kuongeza

“Mbuyu unapong’ooka si shida kupanda mwingine, kati yenu 11 mliobaki mmoja asimame awe mbuyu na mbuyu huo uendelee ukaheshimike.

“Hatutafurahi kuona au kusikia familia ina mgogoro, mnatatizana, nikusihi sana simama kuwa mbuyu wa familia,.,”amesisiitiza Rais Samia.

Aidha, amewasisitiza kuimarisha undungu na mshikamano wa ukoo wa Mwinyi kuendelea kutunza heshima ya Mzee Mwinyi.

error: Content is protected !!