Lissu: Rais hajafanya lolote katika madai yetu

HomeKitaifa

Lissu: Rais hajafanya lolote katika madai yetu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kitaamua kama kiendelee mazungumzo na CCM au la ifikapo mwezi ujao kwa kile wanachodai kuwa mambo mengi wanayolalamikia hayatekelezwi.

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA ( Bara), Tundu Lissu alisema kwa miezi sita sasa kati ya mambo wanayolalamikia katika vikao hivyo, lililotekelezwa ni kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa pekee.

” Tuna majadiliano na CCM, lakini hayajazaa matunda kwenye uendeshaji wa siasa na bado tunaendelea kuzungumza.

“Basically, ukiachilia suala la kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa, Rais hajafanya lolote katika madai yetu,” alisema Lissu anayeishi Ubelgiji.

Lissu alisema kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo, watafikiria vinginevyo katika kikao wanachotarajia kukutana mwezi ujao (Desemba).

“Baada ya miezi sita ya mazungumzo, hatujaona matunda na mwezi ujao tutakutana tuangalie kama tuendelee au tusiendelee,” alisema.

 

 

error: Content is protected !!