Eng. Hersi : Rais Samia anamchango mkubwa kwenye soka letu

HomeKitaifa

Eng. Hersi : Rais Samia anamchango mkubwa kwenye soka letu

Rais wa Timu ya mpira wa miguu ya Yanga SC , Eng. Hersi Said amesema mafanikio katika sekta ya michezo hasa mpira wa kiguu nchini yametokana na mchango mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Alahly kilichopo Cairo, Eng. Hersi Taifa Stars kufuzu kwenda kwenye fainali za AFCON 2023 nchini Ivory Coast ni moja ya jitihada za Rais Samia.

“Chachu ya mafanikio ya mpira wetu Tanzania ni Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu amekuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la nchi yetu.” amesema Eng. Hersi.

Aidha Eng. Hersi amesema mchango wa Rais Samia katika kujenga Hamasa kupitia “GOLI LA MAMA” umeifikisha Yanga SC katika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2022/23 na sasa Yanga SC kufuzu kwenda robo fainali ya Klabu bingwa barani Afrika.

 

 

 

 

error: Content is protected !!