Rais wa zamani wa Angola afariki dunia

HomeKitaifa

Rais wa zamani wa Angola afariki dunia

Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos, ambaye alitawala nchi ya pili kwa uzalishaji mafuta barani Afrika kwa takriban miongo minne, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, ofisi ya rais wa Angola imetangaza kwenye ukurasa wa Facebook leo Ijumaa Julai 8,2022.

Rais huyo wa zamani alifariki saa 11:10 asubuhi kwa saa za Uhispania katika kliniki ya Barcelona Teknon kufuatia kuugua kwa muda mrefu, ofisi ya rais ilisema.

 

 

error: Content is protected !!