Njia 4 za kulishinda jua la Dar

HomeElimu

Njia 4 za kulishinda jua la Dar

Nchini Tanzania katika jiji kubwa la biashara linalofahamika kama Dar es Salaam ni maarufu kwa kuwa na jua kali linalochoma sana huku wengine wakitania kwamba unaweza kunukia kama mshikaki endapo utatembea juani kwa muda mrefu.

Ili sasa kuepuka kunukia kama mshikaki pindi huwapo kwenye jiji la Dar es Salaam basi fanya mambo haya manne;

Kunywa maji mengi

Hakikisha unakunywa maji mengi yakutosha pindi huwapo katika jiji la Dar es Salaam na ikiwezekana tembea na chupa yenye maji. Unashauriwa kufanya hivi sababu unapoteza maji mengi pale jua likikupiga sana na kuanza kutokwa na jasho hivyo ni bora ukanywa maji mengi kufidia yaliyotoka.

Epuka kuvaa nguo za kubana

Usivae nguo za kubana ukiwa unatembea au hata kukaa nyumbani kwani kwa jisni jua lilivyokali mwili unahitaji kupumua zaidi hivyo ni bora ukavaa nguo za kuachia zenye kuruhusu hewa kuingia mwilini.

Usivae nguo zenye rangi nyeusi

Rangi nyeusi huvuta mionzi ya jua kwa wingi hivyo inaweza kukuunguza mwili wako kwa urahisi zaidi pindi utembeapo juani sana. 

Oga maji ya baridi

Baada ya mizunguko ya siku nzima , ukirudi nyumbani hakikisha unaoga maji ya baridi ili kupoza mwili. Pia wakati wakulala hakikisha unajimwagia maji ya baridi na kufungua madirisha hewa iweze kuingia ndai.

 

error: Content is protected !!