Viongozi wa dini wateta haya na Rais Samia kuhusu kesi ya Mbowe

HomeKitaifa

Viongozi wa dini wateta haya na Rais Samia kuhusu kesi ya Mbowe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amezungumza na viongozi wa dini mbalimbali kuhusu maendeleo ya nchi katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wameomba serikali itafakari uwezekano wa kufuta kodi ya mapato kwenye fedha zinazopatikana kama misaada ya hiari ya wanachama na wafadhili kwa ajili ya kuendesha huduma zisizo za kibiashara zikiwemo huduma za wajane na yatima.

Wakati huo huo, viongozi hao wa dini wametumia mkutano wao na Mhe. Rais Samia kuomba mamlaka husika kutumia busara ili kuangalia namna ya kumaliza kesi inayomkabili kiongozi wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.

 

error: Content is protected !!