CHADEMA wamkubali Spika Tulia

HomeKitaifa

CHADEMA wamkubali Spika Tulia

Sophia Mwakagenda ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kwamba wabunge wanaotokana na chama hicho waliamua kumpa kura ya ndiyo Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson baada ya kurudhishwa na utendaji wake wa kazi.

“Sisi wabunge wa CHADEMA tulimpigia kura ya ndiyo, Dk. Tulia ili awe spika kwa wabunge kwa sababu ya utendaji kazi na utashi katika kuongoza vikao vya Bunge. Lakini pia ni mwanamke mwenzetu ilikuwa lazima tumpigie kura,” alisema Mwakagenda.

Aidha, alisema wabunge wa CHADEMA wataendelea kumuunga mkono Spika Dk. Tulia kwa manufaa mapana ya taifa katika kuwaletea maendeleo wananchi kupitia mijadala na hoja mbalimbali ambazo zitakuwa zinawasilishwa bungeni.

Amezungumza hayo katika tafrija ya kumpongeza Dk. Tulia baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa BUnge la Tanzania iliyofanyika jimbobi kwake Mbeya Mjini.

error: Content is protected !!