Kwa wanaume: fanya haya kuzuia kondomu isipasuke

HomeElimu

Kwa wanaume: fanya haya kuzuia kondomu isipasuke

Kwa mwanaume yoyote yule inabidi uwe makini pindi uvaapo kondomu wakati wa tendo la ndoa kwani inaweza kupasuka au kutoka na kubaki kwa mwanamke endapo hautokuwa makini.

Zingatia haya ili uweze kushiriki tendo la ndoa vizuri na kuzuia kondomu kupasuka au kutoka;

Epuka kuweka kondomu sehemu ya joto kali

Unashauriwa kuhifadhi kondomu kwenye sehemu ambapo hakuna joto kali kwani kwakufanya hivyo utasababisha unyenyevu uliokuwepo kukakuka na hivyo kupata nayo shida wakati ukiitumia.

Nunua kondomu saizi yako

Hakikisha unanunua kondomu ambayo inaendana na saizi ya maumbile yako, ukichukua kubwa basi inaweza kutoka wakati wa tendo au ukichukua ndogo inaweza kupasuka hivyo hakikisha unanunua ile itakayo kufaa.

Zingatia uvaaji wa kondomu

Wakati ukijiandaa kushiriki tendo la ndoa, hakikisha unavaa vizuri kondomu ili ikae sawa. Husipoivaa vizuri inaweza ikatoka na kubaki kwa mwanamke au hata kupasuka hivyo zingatia uvaaji wako.

Usivae kondomu mbili

Husivae kondomu mbili wakati unashiriki tendo la ndoa bali moja kwani ukishavaa kumbuka kuna msuguano hutokea hivyo kama umevaa zaidi ya moja lazima itapasuka au uwezekano wa moja kutoka.

Usitumie vilainisha ukivaa kondomu

Usitumie vilainishi kama mafuta ya mgando au ya nazi wakati umevaa kondomu kwakuwa tayari yenyewe inaunyevuunyevu unaotumika kama kilainishi wakati mkishiriki tendo la ndoa , hivyo kuwa makini.

error: Content is protected !!