27 wakamatwa kwa kuiba saruji baada ya lori kupata ajali Mbagala

HomeKitaifa

27 wakamatwa kwa kuiba saruji baada ya lori kupata ajali Mbagala

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata watu 27 wanaotuhumiwa kuiba mifuko ya saruji baada ya malori mawili kupata ajali eneo la Mbagala Mission.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi, Jumanne Muliro imeeleza kuwa juzi 04:30 alfajiri lori aina ya Horse na likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro baada ya tairi kupasuka, ndipo watu zaidi ya 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

   > Bei mpya za mafuta mwezi Oktoba

Aidha, jana saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission lori jingine likitokea Mbagala kwenda mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji lilipata ajali.

‘’Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27 wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye pikipiki na bajaji. Wote walikamatwa, na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu’’ ameeleza.

Kamanda Muliro ameongeza kuwa watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

error: Content is protected !!