Mbinu 5 za kumaliza tatizo la uvivu kazini

HomeElimu

Mbinu 5 za kumaliza tatizo la uvivu kazini

Kama uvivu utapewa nafasi kubwa katika shughuli za kikazi na biashara, hujenga tabia ambayo ikiota mizizi inaathiri kabisa maisha ya mtu. Huenda nawe umekuwa ukijiuliza kwanini mambo yako hayaendi, huenda una tatizo la wa uvivu.

Sasa fanya haya kuepuka uvivu:

1.Ubunifu
Epuka mambo yale yale kila siku. Ichangamshe akili yako kwa kufanya tofauti na ulivyozoea ili kuiamsha, kutafuta namna ya kuendana na mabadiliko katika maisha yako ambapo itakuongezea nguvu ya kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.

2. Kamilisha kazi kwa wakati
Acha kuwa na tabia ya kuwaza kwamba una muda mwingi wa kufanya kazi kwani hali hii itakufanya uwe na viporo vingi na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati.

   > Zijue faida za kula chakula cha usiku mapema

3. Weka malengo ya maisha
Usiishi bila malengo kwani pale unapokuwa na malengo utaacha uvivu na kufanya kazi kwa bidii kwakuwa unatambua nini unatakiwa kufanya.

4. Fanya mazoezi
Kama upo ofisini na unahisi kuchoka basi simama, jinyooshe au hata toka nje ukapate upepo kidgo alafu rudi ndani hii itakupa nguvu ya kurudi kufanya kazi tena.

5. Chagua marafiki wachapa kazi
Unapokuwa na marafiki wanaopenda kufanya kazi watakuhimiza na wewe na hii itaondoa uvivu ndani yako.

error: Content is protected !!