Nauli mpya kutumika rasmi

HomeKitaifa

Nauli mpya kutumika rasmi

Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini(LATRA) Johansen Kahatano amesema kulingana na hali halisi ya upandaji wa bei za mafuta, bei mpya za nauli zilizokuwa zianze kutumika Mei 14, 2022, sasa zitaanza kutumika rasmi.

Gari la matangazo lilipita maeneo ya jiji la Mwanza na kutoa tangazo hilo la ongezeko la bei kwa usafiri wa daladala, huku afisa mmoja wa LATRA ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema kwamba bila kufanya hivyo wamiliki wa magari hayo wangegoma kutoa huduma.

Aidha, alisisitiza kuoanda kwa nauli kumetokana na kupanda kwa mafuta katika mikoa mbalimbali ambayo imesababisha wamiliki wa daladala kulalamika kutaka nauli nayo iongezeke.

hivi karibuni LATRA ilitangaza nauli mpya za mabasi ya mijini, maarufu daladala na mabasi ya masafa marefu yanayokwenda mikoa mbalimbali nchini.

error: Content is protected !!