Zifahamu kompyuta 5 nzuri kutumiwa na mwanachuo

HomeElimu

Zifahamu kompyuta 5 nzuri kutumiwa na mwanachuo

Mbali na kalamu, daftari na kikokotoo, zana nyingine muhimu chuoni ni kompyuta binafsi (laptop) ambayo itakusaidia katika kukamilisha majukumu yako ya kila siku ikiwemo kazi, kuandaa mawasilisho na hata kujisomea.

Siku chache zimebaki kuelekea mageti ya vyuo vikuu nchini Tanzania kufunguliwa ili kuruhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza waanze masomo, hizi baadhi ya kompyuta kwa matumizi bora ya shule vyuo;

Dell XPS 13
Mwanafunzi anahitaji kompyuta ambayo sio nzito ili iwe rahisi kuibeba kwenye begi pamoja madaftari huku gharama yake ni shilingi 3.1 milioni. Mbali na wepesi, kompyuta hii ya uzao (generation) wa 11 ina uhifadhi wa jigabaiti nane hadi 32 (GB8-GB32) ambazo kwa mwanafunzi, zinamtosha. Kwa wanaopenda kuangalia filamu huenda isiwe mahususi.

HP Envy x360
Envy inapatikana kwa shilingi 1.4 milioni huku ikiwa na uwezo wa kukunjika kwa nyuzi 360 na sifa kubwa ya kompyuta hii ni uwezo wake wakukaa na chaji kwa muda mrefu.

Surface Laptop 4
Kuanzia kioo kikubwa na uhifadhi wa hadi GB512, kompyuta hii inaweza kumfaa mwanafunzi kwa kazi hata nje ya chuo huku gharama yake ikiwa ni shilingi 2.3 milioni.

HP Spectre x360
Spectre x360 ni ya uzao wa 11Intel ikiwa na prosesa ya Core™ i5. Inaambatana na uhifadhi wa kuanzia GB8 hadi GB256 pia ina skrini ya kupangusa kama zilivyo simu janja na ukubwa wake ni inchi 13.5.

Acer Swift 3
Ni kompyuta yenye thamani ya shilingi 1.7 milioni inayotumia mfumo endeshi kuanzia Window 10. Mbali na kiandikio (keyboard) kinachowaka, kompyuta hii inamfaa mwanafunzi kwa kuwa na uhifadhi mkubwa wa RAM ya GB8 na uhifadhi wa kawaida wa GB256.

Hizo ni baadhi ya kompyuta zenye uwezo mzuri wa betri na skrini ya kutosha kusomea.

error: Content is protected !!