Mwalimu wa kike ambaka mwanafunzi wa kiume mwenye miaka 15

HomeKimataifa

Mwalimu wa kike ambaka mwanafunzi wa kiume mwenye miaka 15

Loise Martha Musyoka, mwalimu kutoka nchini Kenya Kaunti ya Nairobi wa shule ya Kayole ameshutumiwa kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kiume mwenye miaka 15 mwezi Oktoba 16 mwaka huu nyumbani kwa mwalimu huyo baada ya kumuita ili amsaidie kutengeneza picha za kubandika ukutani.

Mwalimu huyo alimuita mvulana huyo pamoja na wenzake waende nyumbani kwake kumsaidia kutengeneza picha za kubandika ukutani na baada ya kumaliza, Loise alienda chumbani na mwanafunzi huyo alimfuata, ili amrekebishie mtandao na ndio alianza kumbusu, kumvua nguo na kumbaka mvulana huyo.

Uongozi wa shule baada ya kugundua tukio hilo, walimsimamisha kazi Loise kumkataza tabia ya kuita wanafunzi nyumbani kwake ili wamsaidie kazi mbalimbali.
Mwalimu huyo amefikishwa mahakamani lakini amekana mashataka hayo na hivyo kesi yake kupelekwa mbele mpaka mwakani Aprili 4.

error: Content is protected !!