Rais Samia: Sina kabila katika utendaji

HomeKitaifa

Rais Samia: Sina kabila katika utendaji

 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wapya aliowaapisha leo kuacha ukabila katika utendaji wao wa kazi na kusisitiza kuwa suala hilo halina nafasi katika kuwateua viongozi anaowataka.
 
Rais Samia amesema hayo leo Oktoba 11, 2021 mara baada ya kuwaapisha viongozi wateule ambao aliwateua katika nafasi mbalimbali, hafla iliyofanyika leo katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.
 
“Sasa watu wanafanya makosa, ukiwawajibisha, ‘nimewajibishwa kwa sababu ya kabila fulani.’ Sina kabila mimi, hapa ukiniuliza kabila lako nani nitakuambia Mzanzibari. Sina kabila na kwa maana hiyo hata kwenye utendaji wangu wa kazi sina kabila,” amesema Rais Samia.
 
Viongozi walioapishwa katika hafla hiyo ni Sofia Mjema, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Jaji Omar Makungu, kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Jaji Mustapha Siyani, kuwa Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. #clickhabari
error: Content is protected !!