Zawadi ya Messi yamfurahisha Papa

HomeKimataifa

Zawadi ya Messi yamfurahisha Papa

Mchezaji bora wa Dunia mara 6, Lionel Messi amempatia zawadi Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis. Mess amempatia Papa jezi aliyoipiga saini kama zawadi katika sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya kidiplomasia kati ya Ufaransa na Vatican.

Papa na Messi wote ni raia wa Argentina, na inaelezwa kuwa Papa amekuwa shabiki wa mpira wa timu ya San Lorenzo ya nchini Argentina tangu akiwa kijana mdogo.

Jezi hiyo ya PSG yenye nambari 30, iliwasilishwa kwa Papa na Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex jijini Vatican kwenye sherehe za maandhimisho hayo. Papa alionekana mwenye furaha sana wakati akipokea jezi hiyo, kwani inaelezwa kwa kipindi kirefu amekuwa akimshabikia Messi tangu alipokuwa Barcelona.

Katika hali ya kushangaza, Papa aliwahi kukiri mwaka 2015 kuwa, licha ya kumshabikia Lionel Messi, na kukutana naye ana kwa ana mara mbili, lakini hakuwahi kumtazama akicheza mpira. Papa alilieleza gazeti la ‘La Voz del Pueblo’ kuwa ameacha kutazama televisheni tangu 1990 kutoka na nadhiri aliyoiweka alivyoingia maisha ya utawa.

error: Content is protected !!