Tanzania yang’ara kuwa na usalama wa mtandao

HomeKitaifa

Tanzania yang’ara kuwa na usalama wa mtandao

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili katika kielezo cha usalama wa mtandao (GCI) kwa mawaka 2020, wka mujibu wa Shirika la Mawasiliano la Kimataifa (ITU).

Kulingana na taarifa ya ITU, Tanzania imeshika nafasi hiyo kutokana na uimara wake kwenye kukabiliana na matukio ya dharura za usalama katika anga la mtandao. Katika orodha hiyo iliyotolewa na ITU lenye makao yake nchini Uswidi, Tanzania imepata alama 90.58 ikiongozwa na Maurius iliyopata alama 96.89.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Jabir Makame alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na uwezo wa nchi kukabili mashambulizi ya mtandaoni kwa kiwango stahiki.

“Mashambulizi ya anga limekuwa tatizo sugu kwa baadhi ya nchi duniani likisababisha athari katika mifumo ya mawasiliano na tehama na kukwaza jitihada za kukuza uchumi,” alisema Dk Makame.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo baadhi ya vigezo vilivyotumika kupima uwezo wa nchi kukabili mashambulizi hayo ni kupima mikakati ya kitaifa na mashirika yanatotekeleza usalama wa mtandao, ukuzaji wa uwezo unaohusisha kupima kampeni za uhamasishaji, mafunzo, elimu na motisha kwa ajili ya kukuza uwezo wa usalama mtandao na kiwango cha ushirikiano na nchi nyingine, mashirika na makampuni.

 

error: Content is protected !!