Jinsi ya kupata madini ya Almasi kutoka kwenye maiti

HomeElimu

Jinsi ya kupata madini ya Almasi kutoka kwenye maiti

Barani Afrika na maeneo mengine duniani utamaduni wa kuzika mtu anapofariki ni utamaduni wa miaka mingi na ndio utamaduni watu waliuzoea. Lakini kasi ya kukua kwa Sayansi na Teknolojia pengine kuna siku inaweza kuondoa kabisa utaratibu huu kutokana na fursa kubwa inayopatikana kwenye maiti ya binadamu.

Ni wazi kuwa msemo maarufu wa kufa kufaana unafanya kazi kubwa zaidi katika mataifa mengine kuliko huku kwetu Afrika. Nchini Uswisi ipo kampuni inayoitwa Algordanza ambayo kazi yake kubwa ni kuchoma moto maiti kisha kuchenjua jivu la maiti hadi kupata almasi ambayo hukabidhiwa ndugu za marehemu. Kuanzia 2015 nchini Marekani kumekuwa na idadi ndogo sana wanaochangua kuzikwa pindi wanapofariki, watu wengi wamekuwa wakichagua maiti zao kuchomwa moto ili ziwafae ndugu zao.

Unapataje Almasi kutoka kwenye majivu ya maiti?

Mwili wa mwanadamu una madini mengi ya Carbon kuliko madini mengine, na almasi asili yake ni chembechembe za madini ya Carbon. Hata hivyo Wanasayansi kwa miaka mengi wamekuwa wakitafiti juu ya uwezekano wa kuzalisha madini ya almasi kwenye maabara.

Kampuni ya Algordanza imesema inatoa huduma ya kuchoma moto maiti katika mataifa 33, na imefanikiwa kuuza takribani vito 1000 kutoka kwenye majivu ya maiti tangu 2016.

Hatua ya kwanza kuuchoma mwili wa marehemu hadi uwe jivu kabisa, na jivu kati ya kilo 2 hadi 4 litahitajika ili kuanza mchakato wa kupala almasi. Almasi inaweza kupatikana kwa rangi tofauti anayotaka mtu na hata umbo. Majivu yake huchukuliwa na kuweka kwenye kifaa maalumu kutazama kiwango cha Carbon, kisha hutumia aina ya asidi kutenganisha majivu na madini mengine yasiyohitajika kama chumvi na mengine.

Kuna maiti nyingine hutoa almasi yenye ubuluu mwingi kuliko nyingine, hii ni kutokana na kiasi cha madini aina ya boron mwilini. Watu waliopitia matibabu ya Saratani hupigwa mionzi hivyo maiti zao hutoa almasi nyeupe kwa sababu mionzi huondoa madini ya Boron katika mwili wa binadamu wakati wa matibabu.

Majivu yenye Carbon ya kutosha (aslimia 99) huchanganywa madini ya chuma na Kobalt, madini haya huondoa kabisa takataka zisizotakiwa. Ili jivu lenye madini ya Carbon kutoa almasi, lazima lichanganywe na kiwango kidogo sana Almasi halisi, kwani Carbon ya kwenye majivu inafanya kazi vizuri na kujikusanya kama itakutana na kipande cha Almasi halisi.

Gramu 0.06 ya almasi hiyo huuzwa shilingi milioni saba na kampuni hiyo pia imewahi kuuza gramu 0.4 kwa shilingi milioni 110 za kitanzania na kufikia sasa bado oda zinazidi kumiminika. Lakini sio maiti za binadamu pekee ndio zina uwezo wa kutoa almasi, bali hata wanyama kama Mbwa na Paka, hivyo watu wameendelea kupeleka wanyama na ndugu zao kuchomwa wanapofariki ili wawafae maishani.

error: Content is protected !!