CHADEMA yatoa masharti kushiriki kikao na Msajili wa Vyama vya Siasa

HomeKitaifa

CHADEMA yatoa masharti kushiriki kikao na Msajili wa Vyama vya Siasa

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Benson Kigaila amesema kwamba kabla ya kushiriki kikao chochote wanataka zuio ambalo linafanywa na Serikali kwa shughuli halali za vyama vya siasa kuondolewa.

“Kamati Kuu tumekubaliana ili tuweze kushiriki kikao chochote cha msajili lazima zuio la vyama kufanya mikutano ya hadhara yaondolewe, ili tukienda kwenye vikao na msajili twende kama vyama huru, tusiende kama vyama vinavyotoka Mahabusu.” amesema Benson Kigaila.

> Rais Samia: Sina kabila katika utendaji

Aidha, Kigaila amesema CHADEMA kama chama wanaona kwamba Sheria iliyopo pamoja na mapungufu yake inatakiwa kufuatwa na kila mmoja na ndio utaratibu wa kisheria.

“Hatuwezi kukutana na wadau chini ya msajili kujadili changamoto ya kutekeleza hiyo Sheria. Hatutaki kualikwa kwenda kujadili namna ya kuvunja Sheria. Sisi kama chama cha siasa tumesajiliwa na tumejifunza kufuata Sheria na tunaamini utawala wa Sheria,”amesema Benson.

Tarehe 21-22/10/2021 Dodoma Msajili wa Vyama vya Siasa ameitisha kikao cha wadau kitakachohusisha vyama vyote nchini.

error: Content is protected !!