Wilaya 64 kujengwa vyuo vya ufundi stadi

HomeKitaifa

Wilaya 64 kujengwa vyuo vya ufundi stadi

Serikali imesema imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi, katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo hivyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Robert Chacha Maboto, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema serikali imeshakamilisha michoro na upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Akitoa ufafanuzi zaidi leo Aprili 11, 2023 bungeni Dodoma, Naibu Waziri Kipanga amesema Wilaya ya Bunda ni miongoni mwa wilaya hizo, ambazo zipo kwenye mpango huo.

Amesema Sh milioni 45 zimetolewa mwezi Machi, 2023 kwa ajili ya shughuli za awali.

error: Content is protected !!