Fahamu zawadi 5 zitakazofanya mtu akukumbuke

HomeElimu

Fahamu zawadi 5 zitakazofanya mtu akukumbuke

Zawadi ni kitu anachopewa mtu bila matarajio ya malipo kama sehemu ya kumpongeza, kumuunga mkono au kuthamini uhusiano wenu au kitu alichofanya, watu hupewa zawadi wanaposherehekea siku zao za kuzaliwa, wanapofunga ndoa nk kuna zawadi  ndogo ambazo unaweza kumpa ndugu yako, rafiki yako au mpenzi wako lakini zikawa na maana kubwa sana nazo ni ;

Kadi za Zawadi
Inaweza kuwa ni zawadi ambayo imezoeleka sana lakini jaribu kutafuta kadi yenye maneno mafupi mazuri ambayo yamebeba ujumbe kulingana na uhusiano wako na unaempelekea pamoja sababu ya kumpelekea zawadi hiyo, Kitu kingine cha kuzingatia ni rangi na maua ya kadi yako.

Kitu chochote kinachowakilisha kumbukumbu maalum
Mara nyingi picha zinatusaidia kukumbuka nyakati tulizopitia kinabeba kumbukumbu ya mda mrefu, unaweza kumpelekea mtu zawadi ya picha au fremu ya picha au kitu chochote ambacho kitatengeneza kumbukumbu kwenye maisha yake unaweza kumpeleka sehemu nzuri akapate chakula kizuri atakumbuka zaidi kuliko kumpa zawadi ya pipi.

Mapambo
Mtu anaweza kutumia mapambo kuweka kwenye nyumaba yake aua chumba chake na ni zawadi nzuri kwasababu kila atakapokaa ndani kwake ataacha kukumbuka zawadi uliompa, Mapambo yapo ya aina nyingi unaweza kumpa maua ya kuweka ndani picha na michoro ya ukutani lakini pia unaweza kumpa mapambo ya mwilini kama saa, hereni na mkufu.

       > Wanaume: Fahamu meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako kudumisha penzi lako

Vitabu
Maarifa huwezi kuyatoa ndani ya mtu yanaishi ndani yake na kubadili mtazamo wake, kama mtu unaempelekea zawadi anapenda kujifunza jaribu kutafuta kitabu kizuri kwaajili yakekila anaposoma au kutumia maarifa aliyoyapata akupitia hicho kitabu ataacha kukukumbuka.

Mziki
Sio lazima uwe muimbaji ili uweze kumpa mtu zawadi ya nyimbo unaweza kutafuta kanda nzuri ya nyimbo zenye ujumbe unaoendana na uhusiano wenu na ukampatia, nyimbo zinabeba kumbukumbu na ndo maana kuna nyimbo leo zikipigwa watu wanakumbuka matukio mbalimbali waliopiutia aua sehemu walizokuwepo au watu waliokua nao wakati wanasikiliza hizo nyimbo.

error: Content is protected !!