Wafahamu mabilionea 10 wenye utajiri mkubwa zaidi

HomeMakala

Wafahamu mabilionea 10 wenye utajiri mkubwa zaidi

Taasisi mbambali ulimwenguni hufanya utafiti mara kwa mara na kueleza kuhusu utajiri wa watu duniani kote.

Takwimu za mwaka 2021  zinaonesha kwamba dunia ina mabilionea 2,755 (utajiri wao ukipimwa kwa dola za Kimarekani). Katika orodha hiyo, majina 493 yalikuwa mapya, kwa maana kwamba hayakuwemo kwenye orodha ya mabilionea wa mwaka 2020.

Wafuatao ni mabilionea 10 wenye utajiri mkubwa zaidi duniani.

10. Warren Buffet

Anatajwa kama guru wa uwekezaji kutoka nchini Marekani.  Utajiri wake ni dola za Kimarekani bilioni 103.9

9. Steve Ballmer

Aliiongoza kampuni ya Microsoft kuanzia mwaka 200 hadi 2014. Ana utajiri wa dola za Kimarekani 105.6

8. Mark Zuckerberg

Tajiri wa kampuni ya Meta (Facebook) mwenye miaka 36 tu, ana utajiri wa dola za Kimarekani bilioni 119.8.

7. Sergey Brin

Mwaka 2019, Mmarekani huyo ambaye utajiri wake unafikia dola za Kimarekani bilioni 122.3, aliachia kiti chake kama Rais wa kampuni ya Alphabet (kampuni mama ya Google) lakini anaendelea kuwa na hisa nyingi  na mjumbe wa bodi wa kampuni hiyo.

6. Larry Page

Bilionea mwingine kutoka kampuni ya Alphabet, mwenye utajiri wa dola Kimarekani bilioni 127.

Yeye pia anatokea nchini Marekani kwenye sekta ya teknolojia.

5. Larry Ellison

Yuko nchini Marekani akijihusisha na masuala ya teknolojia. Kampuni yake (Oracle) imempatia utajiri usiopungua dola za Kimarekani bilioni 131.

4. Bill Gates

Ni mmiliki wa kampuni ya teknolojia  ya Microsoft ya nchini Marekani, ana utajiri wa dola za Kimarekani bilioni 137.9.

3. Bernard Arnault na Familia yake.

Mfaransa huyo na familia yake wamejikita kwenye mavazi wakisimamia chapa mashuhuri kama Louis Vuitton na Sephora. Utajiri wao ni dola za Kimarekani bilioni 193.6.

 2. Jeff Bezos

Anatokea Marekani, ana utajiri wa dola za Kimarekani bilioni 201.4 alioupata kupitia kampuni ya Amazon inayofanya mauzo kupitia mtandao.

1. Elon Musk

Huyu amejikita kwenye masuala ya usafiri angani na nchi kavu, akifanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hiyo. Anamiliki kampuni ya magari ya Tesla huku kampuni ya SpaceX ikijihusisha na usafiri wa anga.

Ana dola za Kimarekani bilioni 319.9 kibindoni.

Chanzo – Forbes

error: Content is protected !!