Simba na Casablanca, Yanga na TP Mazembe

HomeMichezo

Simba na Casablanca, Yanga na TP Mazembe

Draw za michuano ya klabu bingwa barani Afrika pamoja na ile ya Shirikisho barani humo tayari imekwisha wekwa wazi huku vilabu vya Tanzania vikiangukia kwa vigogo wa soka Afrika, Raja Casablanca ya Morocco pamoja na TP Mazembe ya DRC.

Klabu ya Simba yenyewe imejikuta ikiangukia katika kundi C la michuano ya Klabu bingwa barani Afrika, ambapo itavaana na vilabu vya Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea, pamoja na Vipers ya Uganda.

Yanga wakijikuta ndani ya kundi D la michuano ya shirikisho ambayo ni mashindano ya pili kwa ukubwa baada ya yale ya klabu bingwa. Katika kundi hilo yanga ata sana na vilabu vya Tout Puissant Mazembe ya DRC, US Monastirienne ya Tunisia pamoja na As Real de Bamako ya mali.

Michuano hiyo mikubwa barani Afrika inategemewa kuanza kutimua vumbi katika hatua hizo za makundi mapema februari mwaka 2023.

error: Content is protected !!