Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Rais Yoweri Museveni

HomeElimu

Mambo 8 usiyoyajua kuhusu Rais Yoweri Museveni

  1. Jina lake “Museveni” limetokana na Batalioni ya saba ya jeshi la Uingereza (King’s African Rifles) ambapo ndio kikosi cha Baba yake wakati wa Vita ya Pili ya Dunia.
  2. Ni moja ya Rais msomi Afrika. Ana shahada 3 za Uzamivu (PhD) kwenye Sheria, 2 za fasihi na 1 ya dini. Pia ana shahada moja ya heshima kutoka Chuo Kikuu Cha Faith cha nchini Uturuki.
  3. Ana mtoto mmoja wa kiume ambaye ndiye Mkuu wa Majeshi, Brigedia Muhoozi Kainerugaba. Ana watoto wakike watatu.
  4. Aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi. Alimpindua Milton Obote 1985.
  5. Mwaka 2014 aliweka kamati ya wanasayansi wakubwa kufanya utafiti kwamba ushoga huwa mtu anazaliwa nao, au anajifunza wakati anakua. Mwaka uliofuata akapitisha Sheria ya kifungo cha maisha kwa mashoga.
  6. Amewahi kuachia nyimbo mbili za Rap. Wakati wa kuelekea kampeni za 2011, aliachia wimbo uitwao ‘You want to rap’ na mwaka 2015 akaachia nyingine kwa jina ‘Yengoma’.
  7. Moja ya kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, aliwahi kuwa Daktari wake binafsi.
  8. Museveni ni Rais aliyekaa madarakani muda mrefu zaidi Afrika Mashariki na kati, tangu 1986 hadi leo. Museveni hana dalili ya kutoka na katiba ya Uganda haina ukomo wa madaraka kwa Rais. Aliwahi kusikika akisema, “Nitang’atuka siku Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa nchi moja”

Huyo ndio Museveni, una jingine? Tujuze kwenye comments.

error: Content is protected !!