Kamwe usimwambie mwanaume wako haya

HomeElimu

Kamwe usimwambie mwanaume wako haya

Kuna vitu vingi vinavyoweza kuua mahusiano yako na pengine unajiuliza mara kwa mara ni wapi nimekosea bila kujua namna unavyoongea na mpenzi wako inachangia kwa ukubwa sana kukua ama kufa kwa mahusiano yako.

Ndio wanaume wengi wanajitahidi kuficha hisia zao, lakini yapo maneno ambayo huzigusa hisia zao na kuchukuliwa kama kikwazo cha mahusiano yenu kwenda mbele.

Kwanini usiwe kama…? Kwa ufupi ni kwamba unamlinganisha mpenzi wako na watu wengine na kusahau kuwa hao ni watu wawili tofauti.

Wanaume wanapenda kuwa tofauti na mpenzi wao kuuona utofauti wao na watu wengine hivyo kumlinganisha ni kumfnya ajione kuwa wapo watu wengine ambao wanakuvutia zaidi ya yeye na ungependa awe kama wao.

Kama ambavyo wewe huwezi kuwa kama Amina ama ex wake basi na yeye hawezi kuwa kama ex wako ama watu ambao wewe unataka wafanane. Tafuta maneno mazuri ya kumwambia kuwa ungependa afanye kitu gani badala ya alichofanya, bila kutafuta mfano wa mtu aliyefanya jambo hilo vizuri kuliko yeye.

Hauwezi. Wanaume wengi wanapenda kuonekana wana nguvu za kufanya chochote ikiwepo kumlinda mpenzi wake ama kusaidia shughuli mbalimbali zinazohitaji nguvu.

Anapokuwa anafanya jambo ama anataka kujaribu kubeba kitu na unaona kuwa hataweza kukifanya/kukibeba ni vyema kumwambia kwa ustaarabu labda ngoja nikusaidia upande huu, unahitaji msaada? Hii ni nzito unaonaje akipatikana mtu wa pili mkasaidiana? hiyo ni bora kuliko kumwambia huwezi kunyanyua hicho ama huwezi kufanya hivyo kwani atajiona asiye na nguvu zozote.

Viashiria kuwa mwanamke wako anapanga kuchepuka


Ni mchezo tu.
Usijaribu kuingika kati ya mwanaume wako na na mpira, video game ama aina yoyote ya mchezo anaopenda. hiyo ndio njia yake ya kutulia na kupumzika. Hasa pale unapotaka akatishe mchezo huo na kufanya mambo mengine na wewe kwa kusema ni mchezo tu hata sio muhimu sana.

Yeye anathamini hiyo burudani yake mpe muda wa kufurahia bila vikwazo wala kusema kwamba burudani zake hazina maana. Kama anatumia muda mrefu zaidi ya ulivyotegemea zungumza naye ili aweke muda wake wa michezo bila kusahau muda wake na wewe.

Wewe ni mwanaume, fanya kiume, kuwa kama mwanaume. Kwa ufupi chochote kile ambacho unamkumbusha kuwa yeye ni mwanaume ni chanzo cha michongoma kuota kwenye penzi lenu mapema sana maana wewe bado hujamuona yeye kama mwanaume kamili.

Maneno kama haya yanaweza kumfanya pia kuwa mpenzi mbaya kwako kwani atakuwa anajaribu kufanya vitu kukuonesha kuwa yeye ni mwanaume na kuishia kukuumiza.

Wakati mwingi tumia maneno yasiyomkwaza mwenzio. Tatizo sio kile unachokisema ni vile ambavyo unasema na lengo la kusema hicho ulichosema.

error: Content is protected !!