Mjue mchawi wako sehemu yako ya kazi

HomeElimu

Mjue mchawi wako sehemu yako ya kazi

Unakumbuka wiki ya kwanza ulipoianza kazi unayoifanya? Unakumbuka ulipoipata kazi hiyo uliwaambia watu wangapi na namna ulivyokuwa na furaha? Ilikuwa sherehe moyoni mwako. Kila kitu kilikuwa vizuri, ilikuwa habari njema na baraka kubwa kwako. Lakini sasa kila kitu kimebadilika, unaichukia kwa nguvu zote ile ofisi.

Boss wako anakuandama kila wakati, kila unachofanya kwake hakifai. Muda mwingine anatumia maneno makali yanayokukwaza. Kile kipato ulichokifurahia wakati unaanza kazi sasa hakitoshi kabisa. Hii inakufanya uzidishe chuki yako na unatamani uondoke punde tu ukipata pa kukimbilia. Sio bure, kuna uchawi katika kazi unayofanya. Ndio, uchawi unaoufahamu ila hujatambua chanzo chake.

Ngoja nikuelekeze alipo mchawi wa kazi yako:

  1. Majigambo
    Katika hali ya kawaida inawezekana kweli wewe ndiye unayefanya kazi kwa bidii na unajua vitu vingi kuliko wenzako, sasa zaidi hata ya wale uliowakuta kazini. Kwa Kuwa unafahamu hilo, ullianza kujigamba bila taratibu. Ulitaka wote wafahamu kuwa wewe ndiye kiungo muhimu katika ofisi hiyo na hata Boss wako anakutegemea zaidi wewe.
  1. Kutangaza umeichoka kazi hiyo
    Unapokuwa ofisini, kuna wakati unaona wafanyakazi wenzako kama wote ni rafiki zako hususan pale mnapokuwa mnapiga polojo mida ya ‘lunch’, na ndipo unapojikuta unatoa lawama kwa Watawala au muajiri. Kueleza kuwa huipendi tena kazi hiyo. Habari hizi hufika mbali na muajiri huanza kukuona kama kikwazo kwenye timu yake.
  1. Unadanganya
    Wewe uligeuka kuwa bingwa wa kumpanga Boss wako, unajua nini ukimpiga ‘fix’ ataelewa. Bahati mbaya, Boss wako aliwahi kuwa kwenye nafasi yako kwahiyo anajua. Kubaini kuwa unamdanganya kunamuondolea uaminifu aliokuwa nao juu yako.

     > Fahamu: Kujifungua kwa upasuaji duniani kulianzia Tanzania

  1. Umepoteza uwezo wa kusikiliza
    Kwa sababu unaamini unafahamu vitu vingi, umepoteza uwezo wa kusikiliza maelekezo kama awali. Hivi sasa wewe una uwezo mkubwa zadi wa kueleza. Unaamini unajua mengi na unataka usikilizwe wewe. Wenye uwezo wa kusikiliza zaidi ya kuzungumza huongeza zaidi ufahamu.
  1. Unabeba kazi na sifa za timu kuwa zako
    Unaweza kuwa unajiweka wewe kwenye kazi ambazo hukufanya peke yako na kutaka ionekane kama wewe ndiye uliyefanya zaidi. Kweli, inawezekana kuwa ulifanya wewe zaidi. Kiongozi mzuri ataona wewe unataka kuua vipaji vya wengine na kutaka usifiwe wewe kwanza.

kama dalili hizi zinakuhusu… naamini tayari umeshamjua mchawi wako kazini. Mchawi wako kazini ni ‘Wewe’. Hivyo, unapaswa kubadilika haraka sana kuinusuru ajira yako iwe ya furaha.

error: Content is protected !!