Sherehe za Uhuru kufanyika kimkoa

HomeKitaifa

Sherehe za Uhuru kufanyika kimkoa

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza maadhimisho ya sherehe za uhuru (9 Disemba) yafanyike Kitaifa kwa kuzindua mchakato na kuandikwa kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 – 2050 na kimkoa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo makongamano ya kujadili hatua za maendeleo yaliyofikiwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa taarifa ya Rais wakati akizungumza na maelfu ya wananchi na viongozi wa mikoa na wilaya waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya Bibi Titi Mohammed kwenye viwanja vya Ujamaa, Ikwiriri, wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

“Tarehe 9 Desemba, 2023 ni maadhimisho ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi yetu ambapo mwaka huu Taifa letu litaadhimisha miaka 62. Mwaka huu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameagiza maadhimisho yafanyike Kitaifa na kimkoa,”

“Kila mkoa umeombwa uandae wazee watano maarufu ili waweze kushiriki tukio hilo litakalofanyika Ikulu lakini pia mwaka kesho Muungano wetu utatimiza miaka 60. Kwa hiyo, tunajiandaa na sherehe za miaka 60 ya Muungano ambazo kitaifa zitafanyika Zanzibar,” amesema.

error: Content is protected !!