Fahamu mambo 2 yanayojenga mahusiano imara

HomeElimu

Fahamu mambo 2 yanayojenga mahusiano imara

Mahusiano ni moja ya kitu muhimu sana kwenye mafanikio yetu. Hatuwezi kuwa na mafanikio makubwa bila kuwa na mahusiano mazuri na wengine. Mahusiano yawe mazuri au mabaya yana mchango mkubwa kwenye mafanikio.

Ili tufanikiwe, mahusiano kati yetu na familia zetu yanatakiwa kuwa bora. Kama unafanya kazi na mahusiano kati yako na bosi wako, wafanyakazi wenzako na wateja, yanatakiwa kuwa bora. Kama wewe ni mfanyabiashara, mahusiano yako na wafanyabiashara wenzako, wafanyakazi wako na wateja wako, yanatakiwa kuwa bora pia.

Kwa sababu mahusiano yetu yana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu, leo tujifunze mambo mawili ambayo yatatusaidia kujenga mahusiano bora kati yetu na watu wengine.

Upendo

Bila upendo mahusiano yetu lazima yatapoa, bila upendo mahusiano yetu na wengine yanapoteza thamani. Ni wajibu wako kuwapenda wengine kama unavyojipenda wewe. Ipende familia yako, mpende bosi wako, wapende wafanyakazi wenzako, wapende wateja wako, wapende wafanyabiashara wenzako.

Kama binadamu kila mtu ana mapungufu yake. Kama binadamu kuna kipindi tunakosea. Upendo unapokuwepo ni rahisi sana kwa watu kusameheana pale wapokoseana. Upendo unapokuwepo unaficha madhaifu yetu pia na kutufanya tuishi kwa furaha na amani na watu wengine.

Upendo unawafanya watu wawe karibu zaidi. Kinyume cha upendo ni chuki, chuki inabomoa, upendo unajenga. Chuki inaleta kugombona, upendo unapatanisha. Ili tufanikiwe tunahitaji kupendana bila kuangalia dini zetu, kabila, hata rangi. Tumeumbwa na Mungu kwa kutegemeana ni jukumu letu kupendana na sio kubaguana.

        > Madhara 7 ya kujamiana wakati wa hedhi

Heshima

Tunapaswa kuwaheshimu wengine, mume amuheshimu mke na mke amuheshimu mume, watoto wawaheshimu wazazi na wazazi wawaheshimu watoto. Kila mtu anapenda kuheshimiwa, kila mtu anapenda kuona anapewa heshima kwa vile alivyo na kwa mchango anaotoa.

Heshima sio kwenye familia tu, heshima inaenda mpaka ofisini, biashara, maisha yetu ya kila siku na watu wengine. Ni jukumu letu kuwaheshimu watu wote, bila kujali muonekano wao, jinsia au rangi zao. Bosi muheshimu mfanyakazi, mfanyakazi muheshimu bosi wako. Mfanyabishara ni jukumu lako kuwaheshimu wafanyabiashara, wateja na wafanyakazi wako.

Kama hueshimu mtu usitegemee na yeye atakueshimu. Ili tufanikiwe tunahitaji kueshimu michango ya wengine kwetu. Ni jukumu letu kuwaona wengine wana thamani kubwa na wana uwezo mkubwa na kuwapa heshima.

error: Content is protected !!