Faida 5 za kuwa ‘Single’

HomeElimu

Faida 5 za kuwa ‘Single’

Jana Novemba 11 ilikuwa siku ya watu Single duniani, ni vizuri kuona watu walio kwenye mahusiano wanayafurahi nahusiano yao kila siku, lakini hata watu walio single wana mambo mazuri ambayo watu walio kwenye mahusiano wanayatamani.

1. Utulivu wa kiakili
Kama hauko katika mahusiano, akili yako inakuwa imetuama vyema kwani huna cha kuhofia kama mtu wako anaweza kuibwa na mtu mwingine. Hupati kashikashi ya kupiga simu kila wakati kutaka kufahamu yuko wapi muda fulani na yuko na nani. Hili ni jambo ambalo watu walio kwenye mahusiano wanalitamani lakini hawalipati.

2. Unaweza kutoka (date) na mtu yeyote
Mtoko unaweza kufanya na mtu yeyote ambaye unataka kufanya nae hivyo, sio suala la hadi mtu awe mpenzi wake, la hasha! Hii haiwezekani ukiwa kwenye mahusiano, kwani lazima kuwe na mlolongo wa taarifa kwa mpenzi wako hadi muelewane kwanza. Lakini wasio na wapenzi vichwa vyao ndio serikali zao za kupitisha au kukatisha maamuzi juu yao. Ndio, watu single wanaweza kwenda kokote na yeyote muda wowote.

3. Kulala na mtu yeyote
Hatusemi hili ni jambo zuri, hapana, bali kiwango cha uhuru alicho nacho mtu asiye na mpenzi kinaweza kumpelekea kufanya kitendo hiki. Walio kwenye mahusiano wanaweza kujikaza tu kana kwamba hawaitamani hii hali, lakini fursa hii bahati mbaya wanayo wale wasio kwenye mahusiano pekee

4. Hakuna mawasiliano ya mara kwa mara
Sote tunaelewa mahusiano hujengwa na kitu gani hasa katika karne tuliyomo. Mawasiliano yanavyozidi kupungua kati ya wapenzi basi penzi hapo ujue linaenda josho. Ukiwa huna mpenzi adha unakuwa umeiepuka, japo unaweza kutamani kuwa na mtu wa kukupigia simu kukupunguza upweke, lakini ukweli ni kwamba hali hii watu walio kwenye mahusiano wanaitamani, maana wao ni lazima kila wakati wawasiliane ambapo kuna muda huwa ni kero kwa wengine.

5. Uhuru wa kwenye mitandao ya kijamii
Mtu aingiapo kwenye mahusiano anaanza kujichunga baadhi mambo, hata yale aliyokuwa anafanya awali anayapunguza kwa kiasi kikubwa. Mathalan, kama ilikuwa ni mtu wa masuala ya kupenda sana mitandao ya kijamii basi anaweza kupunguza, ila hii itategemea na aina ya mpenzi uliye nae. Mtu asiye kwenye mahusiano, anaweza kuwa na uhuru kwa kupitiliza kwenye mahusiano kwa kuwa hana wa kumuhofia.

error: Content is protected !!