Mwalimu wa chekechea adaiwa kuwabaka wanafunzi wake

HomeKitaifa

Mwalimu wa chekechea adaiwa kuwabaka wanafunzi wake

Mwanafunzi mwenye umri wa miaka minne anayesoma shule ya awali Pugu Kichangani, Jijini Dar es Salaam anadaiwa kubakwa na mwalimu wake Sekadi Shabani, Mama wa mtoto huyo anadai aligundua mabadiliko ya kiafya ya mtoto wake baada ya mtoto kulalamika maumivu na kuomba apewe dawa.

Mama wa mtoto anasema mtoto huyo alidai kwamba amepata kipele sehemu za siri, Mama anasema alimchunguza mtoto wake sehemu za siri na kukuta ana mabadiliko alipomuuliza mtoto alisema mwalimu shuleni amemfanyia kitu kibaya, lakini pia mtoto alidai kuwa kulikua na wenzie wawili waliofanyiwa kitendo hicho ofisini kwa mwalimu.

“Wakati namchunguza mwanangu nilimkuta na michubuko na alama nyeupe kwenye mapaja yake nilipomuuliza nini kimemkuta aligoma kuniambia ndipo nikamuahidi kuwa nitampa zawadi akinieleza. Mtoto aliongea kuwa mwalimu kamfanyia kitu kibaya.”

Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Pugu kwaajili ya kuangalia afya yake baada ya kufanyiwa vipimo daktari alithibitisha kuwa mtoto alibakwa, majibu ya daktari yalipelekwa katika kituo cha polisi cha stakishari na kupewa RB iliowezeshwa kukamatwa kwa sasa wanasubiri hatua za kisheria dhidi yake.

error: Content is protected !!