Mafuta yaliyosalia nchini yanatosha kwa siku 15 tu

HomeKitaifa

Mafuta yaliyosalia nchini yanatosha kwa siku 15 tu

Shirika la maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) limeweka bayana kwamba mafuta yaliyopo nchini kwa sasa yanatosha kwa matumizi ya siku saba 15 pekee, yaani wiki mbili pekee.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dk. James Mataragio alisema, “Hivi karibuni kumekua na upandaji wa bei ya mafuta na hii inatishia usalama wa nchi, kwa sasa hivi mafuta yaliyopo yanatosha kwa siku 15 tu ikitokea meli haitakuja ndani ya wiki mbili nchi itakua haina mafuta hii sio nzuri kwa usalama wa nchi”.

Magiro alibainisha hatua za dharura zilizochukuliwa ikiwemo ni pamoja na kuagiza mafuta ambayo yanatarajia kuingia nchini muda wowote huku akisema ushiriki wa TPDC utasadia kupungua kwa bei ya mafuta nchini kwani watakua wanayanunua moja kwa moja bila kutumia njia za mkato.

Sambamba na hilo Mkurugenzi Magiro alisema, “Tutahakikisha kunakuwa na mafuta ya akiba ya miezi mitatu, pia tunafikiria kwamba Tanzania tuna bandari na nchi nyingi zilizotuzunguka hazina bandari wanachukua mafuta kutoka hapa, kwa hiyo kutunaweza kununua mafuta na tukawauzia Malawi, Zimbabwe, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) na Zambia.

error: Content is protected !!