Helikopta kutua Mlima Kilimanjaro

HomeKitaifa

Helikopta kutua Mlima Kilimanjaro

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imesema imeridhishwa na miundombinu ya utalii ikiwemo viwanja vya kutua helikopta katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA).

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ally Juma Makoa amepongeza Wizara kwa kuboresha miundombinu katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro akisisitiza “sasa tunaweza kupanda mlima kwa urahisi.”

Makoa amesema Kamati imeridhika na utekelezaji wa miradi hiyo na kumshukuru Rais Samia Suhulu Hassan kwa kuendelea kuipatia fedha Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kuhusu eneo lililokuwa linaungua kwa moto, Makoa amewathibitishia wananchi kuwa moto huo ulishadhibitiwa na Mlima Kilimanjaro kwa sasa ni eneo salama sana na shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema: “Njia hizi mwanzoni zilikuwa zinaleta usumbufu sana na zilikua zinapelekea hata wale wageni wanaopata matatizo ya kiafya wakiwa mlimani, kuchelewa kufikishwa kwenye maeneo ya huduma mjini, lakini kwa sasa wanaweza kupatiwa huduma ya usafiri kwa haraka na kwa urahisi.”

error: Content is protected !!