Afariki dunia baada kunywa pombe bila kula

HomeKitaifa

Afariki dunia baada kunywa pombe bila kula

Asia Eliya (24), Mhudumu wa baa Nyemo amefariki dunia kwa madai ya kunywa pombe kupita kiasi bila kula chakula.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Picha ya Ndege, Joseph Zambo alisema kuwa Asia alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

“Nilipigiwa simu kuwa kuna mwili wa mtu aliyekufa ilibidi niende na nilipofika niliambiwa mwili umechukuliwa na polisi kupelekwa Tumbi ambapo alikuwa hajafa na alifia njiani,” alisema.

Alisema kuwa wafanyakazi wenzake walisema kuwa siku hiyo Asia alikunywa sana pombe kabla ya umauti kumkuta.

“Alichunguzwa lakini hakukutwa na jeraha lolote wala kuumia popote, hali ambayo inaonesha kuwa inawezekana pombe ndiyo ilisababisha kifo hicho,” alisema Zambo.

 

error: Content is protected !!