Ifahamu mikoa 14 nchini hatarini kupata ukame

HomeKitaifa

Ifahamu mikoa 14 nchini hatarini kupata ukame

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dk. Agnes Kijazi amesema utabiriki unaonesha mikoa 14 nchini ambayo ni Mtwara, Lindi, Dodoma, Singida, Njombe, eneo la Kusini la Kigoma,Rukwa, Tabora, Songwe, Mbeya, Katavi, Ruvuma, Iringa na Morogoro itakuwa na upungufu wa mvua ambapo kwa kawaida mikoa hiyo kila mmoja una msimu mmoja tu wa mvua kwa mwaka.

“Utabiri wetu unaonesha upungufu mkubwa wa mvua katika maeneo yanayopata msimu wa mvua mara moja kwa mwaka yaani mikoa ya Magharibi mwa nchi yetu na Kusini, lakini pamoja na utabiri huu kuonesha upungufu wa mvua katika maeneo hayo, upo pia uwezekano wa vipindi vifupi kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo tajwa,” amesema.

> Kauli ya Waziri Mkuu dhidi ya Chanjo Uviko-19

Kutokana na utabiri huo, TMA imepata fursa ya kukutana na wadau wa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, mazingira, nishati na mamlaka za maafa kadhalika sekta ya uvuvi, maliasili na utalii, ujenzi na uchukuzi ambao kwa pamoja wametoa tahadhari kwa jamii kuchukua hatua stahiki kukabiliana na matokeo ya hali hiyo.

Dk. Kijazi amesema wakulima wanatakiwa kuhakikisha wanapata ushauri wa maofisa ugani kwenye kila hatua wanayoifanya katika shuguli zao wakati huu pamoja na kulima mazao yanayostahamili ukame na yanayokomaa kwa muda mfupi.

error: Content is protected !!