Wito wa Rais Samia kwa Majaji na Mahakimu

HomeKitaifa

Wito wa Rais Samia kwa Majaji na Mahakimu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Majaji na Mahakimu wote kutumia kitabu kipya cha ‘Tanzania Gender Bench Book On Women’s Right’ kama mojawapo ya mwongozo itakayotumiwa mahakamani katika kushughulikia mashauri mbalimbali.

“Wito wangu kwa Majaji na Mahakimu wote wanaoshughulikia mashauri ya kutelekezwa mirathi, dhuluma, uzalilishwaji na unyanyasaji kutumia kitabu hiki miongoni mwa miongozo itakayotumiwa.” alisema Rais Samia

Amesema hayo katika uzinduzi wa kitabu hicho kilichoandaliwa na Chama cha Wanasheria na Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA).

Aidha, alifafanua lengo la kitabu hicho ni kuhakikisha utu na heshima ya Mwanamke inalindwa na kuweka wazi haki za Wanawake zinazofahamika na zisizofahamika na watu wengi.

error: Content is protected !!