Fahamu: Kujifungua kwa upasuaji duniani kulianzia Tanzania

HomeElimu

Fahamu: Kujifungua kwa upasuaji duniani kulianzia Tanzania

Wakunga kutoka Tanganyika (Tanzania ya sasa) mwa Ziwa Victoria walishabobea kuzalisha kwa upasuaji miaka takribani 100 hata kabla sayansi ya sasa kugundua kuwa inawezekana mjamzito kuzalishwa kwa upasuaji.

Pindi mjamzito anaposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida, Wakunga walitumia upasuaji wa kimila ambao kwa miaka mingi wameweza kuzalisha bila matatizo. Kwanza walitengeneza mvinyo wa asili kwa kutumia migomba na kutumia kama ganzi wakati wa upasuaji ili mjamizto asisikie maumivu.

Kisu kikali mno kilitumika kuchana sehemu ya chini ya kitovu, lakini kisu kile walikikanza kwenye moto wa wastani kuua vijidudu ambayo vingeweza kusababisha matatizo kwenye kidonda cha upasuaji. Utaalamu huu ulisaidia sana kufanya wajawazito wengi wajifungue salama bila matatizo.

Baada ya mtoto kuzaliwa, dawa maalumu za kimila zilitumika kusafisha kidonda na eneo zima kisha kushonea kidonda kwa ustadi mkubwa bila kumdhuru mzazi. Wanahistoria wanaeleza kuwa ilikuwa aghalabu sana kwa wajawazito kupoteza damu nyingi au kupata maambukizi yeyote, isipokuwa, tatizo ambalo liliripotiwa mara kwa mara, ni maziwa kuchelewa kutoka kwa mjamzito.

Kwa Uganda, Ukunga huu wa jadi ulifanywa na Wanaume, lakini kwa Tanzania na DRC, kazi hii ilifanywa sana na Wanawake. Wazungu walipofika mwanzoni mwanzoni mwa 1800 walishangazwa sana na kitendo hiki na wakahoji namna kinavyofanyika.  Wakunga kutoka Tanganyika na Uganda walisema kuwa utaalamu huu wamerithi kutoka kwa mababu zao miaka dahari iliyopita.

Wakati huo Ulaya ndio wameanza kugundua kuosha mikono kwa maji ya kawaida kabla ya kufanya upasuaji, nusu ya Wanawake Ulaya na Marekani walifariki wakati wa uzazi wa kawaida, na asilimia 100 wa Wanawake walifariki pindi walipojaribu kufanya upasuaji kwa njia ya upasuaji. Utaalamu wa kijadi kutoka Uganda ulianza kuchapishwa kwenye majarida katika kipindi cha kuanzia miaka ya 1880 na ilisaidia nchini nyingi sana duniani kuwezesha Wanawake kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Utaalamu huu ulitapakaa sana miongoni mwa makabila ya Wahaya waishio pembezoni mwa Ziwa Victoria kwa upande wa Tanganyika na Uganda. Hata kule DRC walikuwapo watu wenye stadi hii iliyoleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya afya ya uzazi.

error: Content is protected !!