Wavuvi Ziwa Victoria kupewa mafunzo wa uokoaji

HomeKitaifa

Wavuvi Ziwa Victoria kupewa mafunzo wa uokoaji

Kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila la kuwapa mafunzo wavuvi wanaofanya shughuli zao kando ya Ziwa Victoria, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza ofisi yake kuhakikisha vijana hao wanapata mafunzo ya uokoaji.

“Namuagiza katibu mkuu wa wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia kitengo hiki kwa ombi la Mkuu wa Mkoa la kuwapa mafundisho hawa aje hapa mara moja, apate lile kundi la wavuvi waliokuwepo pale jirani walioshuhudia tukio na kuanza kusaidia ili waone namna ya kuwawekea vizuri ushirika wao wavuvi ili wawaendeleze kwa kupata mafunzo,” amesema Waziri Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa kijana Majaliwa aliyejitosa ziwani na kufungua mlango wa ndege uliowawezesha watu waliokuwepo ndani kutoka, pia Rais Samia Suluhu ameagiza kijana huyo kuingizwa kwenye jeshi la uokoaji na kupewa nafasi.

error: Content is protected !!