Rais Samia: Msiijadili tu serikali

HomeKitaifa

Rais Samia: Msiijadili tu serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassana ametoa wito kwa vyama vya siasa kukaa na kujijadili namna vyama hivyo vinavyotenda kazi.

Amesema hayo, wakati akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Kaeni mjijadili na msijadili tu serikali inavyoendesha shughuli za siasa lakini wakati wa kujijadili na nyinyi wenyewe nani anafanya nini, tunakwenda vipi kwenye siasa zetu.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema serikali imepokea mapendekezo yote ya kikosi kazi na kuahidi kuyapitia ili wayafanyie kazi.

error: Content is protected !!