Rais Samia aizawadi Zambia Hecta 20 Bandari Kavu ya Kwala

HomeKitaifa

Rais Samia aizawadi Zambia Hecta 20 Bandari Kavu ya Kwala

Rais Samia Suluhu Hassan aigawia Zambia hecta 20 za ardhi katika bandari kavu ya Kwala kama zawadi ya kutimiza miaka 59 ya uhuru wao.

Amesema taarifa hiyo aliposhiriki maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia.

“Kwa dhamira ya kuwa watu katikati ya jitihada zetu na kulingana na malengo yetu ya kurahisisha biashara kati ya nchi zetu mbili, serikali yangu imeamua kutenga hecta 20 za ardhi katika Bandari Kavu ya Kwala iliyoko Mkoa wa Pwani nchini Tanzania kwa ajili ya bidhaa zinazokwenda Zambia.” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amesema, Zambia itanufaika kwa muda mrefu na eneo hilo kwa kuhifadhi bidhaa hatua ambayo itapunguza kucheleweshwa na kupunguza gharama za biashara nchini humo.

Rais Samia yupo nchini Zambia kwa Ziara ya Kiserikali ya siku tatu ambapo kesho anatarajiwa kuhutubia katika bunge la nchi hiyo.

 

 

error: Content is protected !!