Jela miaka 60 baada ya kumbaka mama miaka 56

HomeKitaifa

Jela miaka 60 baada ya kumbaka mama miaka 56

Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma imemhukumu kifungo cha miaka 60 jela, Daudi Samson (22) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka na kumlawiti mwanamke mwenye umri wa miaka 56 na kumsababishia maumivu maklai ikiwamo kumvunja mgongo.

Mlalamikaji aliileza mahakama kuwa alimtambua aliyemtendea ukatilii huo na kumtaja kwa majina na kwamba wakati akimbaka na kumlawiti alikuwa akitishia kumuua kwa kumchinja kwa kutumia kisu alichokuwa amekishikilia.

“Nililia sana nikamwambia Daudi kwa nini unanifanyia haya katika utu uzima wangu huu nilionao,wewe si ni sawa na wanangu? Lakini hakunihurumia, aliendelea tu huku akinitaka ninyamaze la sivyo angeniua,” alisema mama huyu wakati alipotoa ushahidi wake.

Aidha, mshatakiwa wakati akijitetea alikana kutenda makosa hayo na kwamba hata mashahidi waliomtaja walitumia maneno ya kusikia kwa mlalamikaji, kwa upande wake hakupeleka shahidi hata mmoja.

Akisoma hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Stanley Mwakihaba alisema upande wa mashtaka ambao jana uliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Tawabu Issa, ulipeleka mashahidi watano ambao walisikilizwa miongoni mwao ni dakatari aliyemhudumia mlalamikaji. 

error: Content is protected !!